Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa смотреть последние обновления за сегодня на .

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji kwa Njia ya Kisasa

54182
351
45
00:08:01
25.07.2021

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji kwa Njia ya Kisasa 🤍fursatv Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi sana, na kila anaye vutiwa kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji anatamani kufanya ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa. Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa hauna faida kwa sababu zifatazo:- 1. Gharama ya uendeshaji iko juu sana ukizingatia unapaswa kuwahudumia kwa kila kitu 2. Usipo walisha chakula chenye virutubisho vyote muhimu watapunguza uzalishaji na vifaranga hawata kuwa vizuri 3. Kuku wa kienyeji wakifugwa kwa njia ya kisasa wapata msongo ambao pia hupunguza uzalishaji wa mayai. #changamkiafursa2021 #kukuwakienyeji

ULEAJI WA VIFARANGA WA KIENYEJI KWA NJIA YA KISASA

262348
3024
254
00:10:27
07.03.2020

Uleaji Bora wa Vifaranga wa kienyeji Wafugaji wa kuku wa kienyeji, wengi hulifanikisha zoezi la ukusanyaji wa vifaranga wengi wa kienyeji kwa njia rahisi. Changamoto kubwa kwao ni uleaji wa bora wa vifaranga. Kwenye video hii tutajifunza Uleaji wa vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa. kwa sababu bila kuwa na elimu ya ufugaji wa kuku vifo vingi hutokea na Wafugaji hukata tamaa. Ili Kujifunza zaidi tafadhali tazama video hii 🤍

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji - Muongozo kwa Wanaoanza Ufugaji

94390
899
63
00:14:05
06.03.2021

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji - Muongozo kwa Wanaoanza Ufugaji Kuku wa kienyeji wakifugwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni bora za ufugaji wa kuku, wanaweza kuwa chanzo cha mapato na kuinua kipato cha familia. Vilevile wanaweza kupunguza tatizo la lishe kwa kuzalisha mayai na nyama isiyokuwa na madhara. SUBSCRIBE: 🤍 Zifatazo ni hatua za ufugaji bora wa kuku wa kienyeji:- 1. Kutafuta elimu ya ufugaji bora wa kuku, elimu ambayo itakusaidia kupunguza changamoto za magonjwa na vifo. 2. Kuchagua Mfumo wa kufugia na Kujenga banda la kuku Kati ya mifumo mitatu ya ufugaji wa kuku, mfumo wa huria au nusu ndani nusu nje ndio mifumo mizuri kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. 3. Chagua mbegu bora ya kufuga Uchaguzi wa mbegu bora ni moja ya vitu vya kuzingatia kwenye kwenye ufugaji wa kuku. Kwenye kuku wa kienyeji nikisema mbegu bora namaanisha uchague kuku ambaye anajiuza atakapo ingia sokoni yaani kuku mwenye umbo kubwa na uzito unao takiwa. 4. Kuandaa vifaa vya chakula na maji vya kienyeji ili kupunguza gharama za uanzishaji wa mradi. Vifaa vya chakula na maji ni muhimu sana kwenye udhibiti wa Magonjwa ya kuku hasa yanayosambaa kupitia uchafu unaotoka kwa kuku mgonjwa. 5.Kuandaa chakula cha kuwalisha kuku wako. Katika suala zima la chakula na jinsi ya kuwalisha kuku wa kienyeji wengi huwa wanafanya makosa. Makosa ambayo hawapelekea kuikosa faida waliyokuwa wakitegemea kuipata wakati wa mavuno. Wengi hupata hasara kwa sababu ya gharama za chakula zinaenda juu zaidi ya faida inayopatikana. 6. Kusanya Makoo/tetea na jogoo kwa idadi unayoweza kumudu kuwahudumia. Nenda vijijini, kusanya Makoo/matetea na jogoo kwa idadi unayohitaji kuanza nayo. Zingatia ubora wa kuku kama tulivyozungumza kwenye sehemu ya kwanza. 7. Uchunguzi wa Magonjwa na tiba Baada ya kuwafikisha kuku bandani, tenga muda wa wiki 2 za kuwachunguza ili kubaini kama wanamaambukizi yeyote ya ugonjwa. 8. Utagaji na utamiaji wa mayai Tengeneza viota vinavyoendana au kuzidi idadi ya tetea uliowanunua ili kuepusha kuku zaidi ya mmoja kutagia kwenye kiota kimoja, na ikitokea wametaga kiota kimoja tenganisha kila yai kiota chake. Pia kama unaweza kutenganisha sehemu ya kulala na kutagia itakuwa ni vizuri zaidi maana kuku wanaoatamia hawata sumbuliwa. 9. Uleaji wa vifaranga Uleaji wa vifaranga ni kipengele muhimu sana kwenye ufugaji wa kuku. Kuna vitu vya kuzingatia wakati wa uleaji wa vifaranga I. Aina ya chakula unachowalisha II. Utaratibu wa chonjo muhimu III. Usafi wa vyombo ya chakula na maji IV. Ukubwa wa banda uendane na idadi ya vifaranga V. Kutibu kwa wakati mripuko wa magonjwa ya coccidiosis, pullorum, typhoid n.k 10. Kuendeleza kizazi Kitu muhimu ni kuhakikisha unakuza vifanga wengi ili uwe na wazazi wengi wa baadae. Ili kuendeleza kizazi unapaswa kuhakikisha kuwa, vifaranga walionguliwa wakifisha umri wa kupandwa hawapandwi na baba au kaka zao. PLAYLIST Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji 🤍 Magonjwa ya Kuku Bofya link kutazama video hizo 🤍 Uleaji wa vifaranga vya kuku Kwa Kutumia Brooder 🤍 Instagram 🤍instagram.com/Changamkiafursatv What's spp +255752209073

TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI:Mambo matano muhimu ya kufuga kuku wa kienyeji kisasa

24703
103
18
00:04:55
08.08.2021

UTAJIRI WA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI UFUGAJI KUKU WA MFUMO WA NDANI Kuku hujengewa banda rasmi na ufugaji wa kuku hufanywa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa. FAIDA Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku pia Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine. HASARA Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU. 1. Matandiko yageuzwe kila siku 2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia. JINSI YA KUANZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI NJIA YA KUPATA KUKU WENGI WA KIENYEJI KWA MUDA mfupi SHAMBANI: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI JINSI YA KUANZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI HATUA kwa hatua UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI MAHITAJI Ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili) KUKU WA KIENYEJI: Mtaji mdogo ila pato ni maradufu UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KWA NJIA ZA KISASA Fomula ya ufugaji bora wa kuku wa kienyeji - Funguka Tanzania Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija Wajua kuku wa kienyeji ni utajiri kuliko wa kisasa? Jinsi Ya Kufuga Kuku wa Kienyeji na Faida zake Tanzania aina za kuku wa kienyeji utajiri wa kuku wa kienyeji yai la kuku wa kienyeji soko la kuku wa kienyeji chakula cha kuku wa kienyeji ujenzi wa mabanda ya kuku wa kienyeji pdf kuku wa kienyeji hutaga mayai mangapi chakula cha kuku wa kienyeji pdf #mkulimasmart #shambadarasa

Fuga Kuku Wa Kienyeji Wa MWENDOkasi Wanalipa Sana.

1616
11
8
00:07:31
13.08.2023

Jiunge Na Group letu la Mwendokasi 🤍 WAFAHAMU KUKU WA AINA YA MWENDOKASI WANAOZALISHWA NA KUKU VILLAGE* MWENDOkasi ni kuku Aliyeboreshwa Mwenye asili ya Kienyeji wa Tanzania (ambao ni Kienyeji wa Kisukuma pamoja na Kienyeji wa Horas. Lakini akafanyiwa Uborashaji Zaidi ili kumuwezesha Kuwa na Uwezo wa Kutaga Sana na Awe Anakua Haraka, ili afae kwa nyama pia. Ni mbegu ambayo hukua haraka sana, hutaga mayai 250 na kuendelea kwa mwaka, ni kuku ambao wana nyama tamu zaidi ya Kienyeji wa kawaida, ni kuku ambao wanastahimili magonjwa na ni kuku ambao wanakuwa na Nyama nyingi na maumbo makubwa bila kusahau huweza kufikisha hadi kilo 5 ndani ya miezi 6 au 7. Kuku wa MWENDOkasi ni kuku wanaopatikana kuku village pekee kwani wao ndiyo waliofanya utafiti wa mbegu hiyo na kupata aina , muonekano na sifa za kuku hao ambao kutokana na sifa zao za ukuaji na utagaji walipewa jina la *_MWENDOKASI_* Lengo la kupata MWENDOkasi lilikuwa ni kuangali namna tunaweza ingia sokoni na kuku bora anayekua haraka, Mrefu , Mstahimilivu wa Magonjwa, Mtagaji sana, anayetaga Mayai Meupe, Medium Size na yaliyochongoka, na bado akipata hizo sifa zote asipoteze ladha, na muonekano wa wa Kuku wa Kienyeji . Ndiyo maana tukapata *MWENDOkasi.* Kiufupi tunaweza sema _MWENDOkasi ni kienyeji wa kibiashara ._ Kwani malengo ya Kumzalisha ni kuchukua nafasi pana ya Kuku wa Kienyeji katika Utagaji zaidi na ukuaji zaidi bila Kuathiri Ubora Wa kuku wa Kienyeji. Kingine MWENDOkasi anafugika katika mazingira yoyote, iwe ndani, huria na nusu huria. Pia ukimfugia nje akapata Majani ya kutosha huwa anakuwa na Nyama na Mayai ya njano. Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa katika soko la kuku, kuku wa kienyeji ni dhahabu, hasa mijini. Kwani ana bei kubwa na hapatikani kwa wingi. Sasa wewe utakayefuga MWENDOkasi hii itakuwa ni faida kwako kwani utazalisha kuku wengi sana, na utawauza kwa bei ile ile ya juu. Hivyo kufanikiwa zaidi kibiashara . Pia kuna kitu ambacho wafugaji ni lazima wajue. Katika ufugaji ili upate matokeo bora ni lazima ufuge kitaalamu. Yani Chakula Bora, Chanjo, Usafi na biosecurity . Hivi vitu vitakusaidia ufike vizuri katika malengo yako. Jambo la msingi unalotakiwa kufahamu... ukifuga MWENDOkasi mpaka anafikisha miezi 4 au 5. Gharama zitakuwa around 3000* Mpaka 7000 * (gharama zitategemea na eneo ulilopo) kwa kuku na ukimuuza ni kuanzia 10,000 Mpaka 25,000 inategemea na mahali ulipo. Pia mayai yake utauza 10,000 mpaka 18,000 Kwa Trei. Kuku wetu wa MWENDOkasi, wanafikia umri wa kuliwa au kuuzwa kwa nyama wakiwa na miezi 2.5 mpaka 3, huku wakiwa na uzito wa 1.8kg kwa tetea na 2.3 kwa jogoo. Kwa upande wa mayai kuku wa MWENDOkasi huanza kutaga wakiwa na wiki 18 yaani miezi 4.5. Na wakifikia peak ya utagaji huwez kutaga kwa asilimia 82 mpaka 88. Viwango ambavyo ni vya _COMMERCIAL LAYERS_ Kwenye Suala la kulalia kuku wetu wamegawanyika katika makundi mawili wapo wanaolalia na wasiolalia.. kwasababu Lengo la kupata MWENDOkasi ni sababu za biashara ya Mayai basi kuku wanaolalia huwa ni wachache. Na hii lengo lake ni kuwasaidia wanaohitaji Vifaranga na hawana mashine basi watatumia hao tetea katika kuatamia na kupata Vifaranga. Ila kama mteja atahitaji kuku wengi zaidi walalie basi kuku wetu huwa wanatabia ya kuambukizana tabia ya kulalia. Akiwaacha hao wanaolalia kwa muda mfupi atajikuta kuku karibia wote wameingia joto na kulalia. Ila kwa wale wateja wasiohitaji kulali . Huwa kuna namna ambayo huwa tunawashauri wafanye ili kuondoa hiyo hali na kumuepushia mteja hasara ya kulalia na kukata utagaji.

Uleaji wa Vifaranga wa Kuku wa Kienyeji Kwa Njia ya Kisasa

32972
295
76
00:13:46
07.04.2021

Uleaji wa vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa Tukuachilia mbali mbinu ya zamani ya uleaji wa vifaranga wa kuku wa kienyeji, wafugaji walikuwa wanashindwa kuendeleza mradi kwa sababu ya vifo vingi vya vifaranga. Ili kuhakikisha mradi unakuwa, mfugaji unapaswa kulea vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa. Vitu muhimu kwenye uleaji wa Vifaranga wa Kienyeji kwa Njia ya Kisasa 1. Banda la kulelea Vifaranga wa kienyeji 2. Vifaranga vya chakula na maji ndani ya banda la Vifaranga 3. Walishe Chakula cha vifaranga chenye virutubisho vyote 4. Zingatia usafi wa vyombo na banda la Vifaranga 5. Wape antibiotics na chanjo kwa wakati. Kwa muda wote huo unaweza ukatumia Neoxychick formula au otc 20 na vitamin, Amprollium. #uleajiwavifarangawakienyeji

USHAURI KWA WANAOTAKA KUANZA UFUGAJI WA KUKU

97307
872
70
00:04:47
02.06.2020

Kabla ya Kuanza Ufugaji wa Kuku wa Aina yeyote, kuku chotara, kuku wa kienyeji, kuku wa mayai, kuku wa nyama Unapaswa Kuzingatoa mambo ya fatayo Utafiti wa aina gani ya kuku ufuge Elimu ya ufugaji bora wa kuku unayotaka kufuga Ujenzi wa banda bora la kuku Mtaji wa kuendeshea mradi wako PLAYLIST Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji 🤍 Ufugaji wa Kuku Chotara 🤍 Magonjwa Tishio ya Kuku 🤍 Ujenzi wa Banda Bora 🤍 Uleaji Bora wa Vifaranga 🤍 SOCIAL MEDIA YouTube; 🤍 Facebook; 🤍 Instagram; 🤍 Twitter; 🤍 What's app; 255 (0)752209073 For Advertisements Email; changamkiafursa🤍gmail.com

JINSI YA KUANZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

242447
1281
98
00:06:41
07.09.2019

jinsi ya kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji Mafanikio kwenye ufugaji wa kuku hayaji kama chafya, zipo hatua mbalimbali ambazo zipaswa kufatwa ili kufanikiwa kwenye ufugaji wa kuku. Hatua hizi ni 🐓👇 1. Elimu bora ya ufugaji wa kuku 2. Utafiti na uchaguzi wa aina gani ya kuku ufuge 3. Ujenzi wa banda bora la kuku 4. Kusafisha banda na kwaajili ya kupokea vifaranga 5. Kupokea vifaranga na kuanza kuvilea

JINSI YA KUPATA PESA KWA HARAKA KWA KUKU WA ASILI/KIENYEJI TU

25271
345
82
00:09:39
21.01.2023

Jinsi ya kupata faida kwa kuku wa kienyeji. Faida HADI Mil. 2 kwa kuku wachache tu 44 na kwa miezi 6 tu #tibaasili #chakulachakuku #magonjwayakuku Jifunze jinsi ya kuchanganya chakula cha kuku kupitia 🤍

JINSI YA KUPATA KUKU 100 WA KIENYEJI KWA MIEZI 3 TU

33565
275
254
00:10:29
03.11.2021

Mbinu za kupata kuku 100 wa kienyeji kwa muda mfupi. Anza na kuku 12 tu ndani ya miezi 3 utapata kuku zaidi ya 100 #kuku#kienyeji#ufugaji 👉Jinsi ya kupata kuku bora wa kienyeji kwa ajiri ya kuanza ufugaji 🤍 👉Vyakula vya kuku kutaga mayai mengi, makubwa na yenye kiini cha njano🤍 👉Ujenzi wa banda la kuku 🤍 👉Chanjo ya ndui 🤍 👉Tiba asili za kuku mimea 12 🤍 👉Ugonjwa wa mafua kwa kuku 🤍 👉Mbinu za kupata kuku wengi 🤍 👉Jinsi ya kulea vifaranga 🤍 👉Jiunge nasi telegram /Follow us Telegram via 🤍 🙏🙏🙏

NJIA YA KUPATA KUKU WENGI WA KIENYEJI KWA MUDA MFUPI 2021

255596
2286
192
00:12:11
07.04.2020

Njia Rahisi ya Kupata Kuku Wengi Wa Kienyeji Kwa Muda Mfupi 2021 Tunahitaji kumuinua mfugaji wa kuku wa kienyeji aache kuishi na kuku na aanze kufuga kuku wa kienyeji kibiashara. Ili ufuge kuku wa kienyeji kibiashara unatakiwa kuwa na makoo yasiyopungua 250. Sio rahisi kwa Wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho. Ili Kujifunza zaidi tafadhali tazama video hii 🤍 Sasa ili kulikamilisha hilo mfugaji anapaswa kuwa na uwezo wa kuzalisha vifaranga wengi kwa pamoja, ambavyo vitampa mfugaji hamasa ya kuweka nguvu kubwa kwenye uleaji wa hao vifaranga kitu ambacho kitachangia ongezeko kubwa la idadi ya kuku na kuleta tija kibiashara. Kufanikisha zoezi hili mfugaji anapaswa kuandaa vitu vifuatavyo:- 1. Banda bora na litakalo endana na idadi ya kuku anaohitaji kufuga. 2. Makoo 20 na jogoo 3 - 4 (Makoo ni kuku ambao wametaga angalau mara moja). Makoo watasaidia kupunguza muda wa kusubiri ili kuliona yai la kwanza. 3. Vifaa vya maji, chakula, joto na bruda 4. Chumba maalumu cha kulelea vifaranga 5. Makasha ya kutunzia mayai 6. Elimu ya ufugaji bora wa kuku, itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za mradi wako Baada ya kukamilisha maandalizi hayo, sasa twende tukaanze kuzihesabu hatua za awali za kufata ili kukusanya vifaranga wengi kwa pamoja na baadae uleaji wa hao vifaranga watakaokuwa kuku wa baadae PLAYLIST Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji 🤍 Ufugaji wa Kuku Chotara 🤍 Magonjwa Tishio ya Kuku 🤍 Ujenzi wa Banda Bora 🤍 Uleaji Bora wa Vifaranga 🤍 SOCIAL MEDIA YouTube; 🤍 Facebook; 🤍 Instagram; 🤍 Twitter; 🤍 What's app; 255 (0)752209073 For Business Purposes Email; changamkiafursa🤍gmail.com

Ushauri wa Mama Lymo kwa Anae Anza Ufugaji wa Kuku Chotara

26276
220
39
00:09:36
24.05.2023

Ushauri wa Mama Lymo kwa Anae Anza Ufugaji wa Kuku Chotara

Chanjo ya Vifaranga vya kuku - Kuku wa Kienyeji, Chotara na Kuku wa Kisasa

126631
697
90
00:11:01
27.08.2018

Chanjo ya vifaranga vya kuku Ufugaji wa kuku kwa nchi za Africa mashariki zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda unaendelea kukua kwa haraka licha ya changamoto za magonjwa ya kuku kuathiri zaidi biashara hiyo. Changamkia fursa inashauri wafugaji wa kuku kufuata ratiba sahihi ya chanjo kwa vifaranga vya kuku ili kupunguza changamoto hizo kama ifuatavyo :- 1. Chanjo ya mdondo / Newcastle (siku ya 7) 2. Chanjo ya Gumboro (siku ya 14) 3. Chanjo ya mdondo /Newcastle 2 (siku ya 21) 4. Chanjo ya Gumboro 2 (siku ya 28) 5. Chanjo ya ndui (siku ya 35) Baada ya hapo mfugaji atarudia chanjo ya mdondo kila baada ya miezi 3 #chanjoyavifarangawakienyeji #ufugajiwakukuwakienyeji #changamkiafursatv

NJIA YA KUPATA KUKU WENGI WA KIENYEJI KWA MUDA MFUPI

248375
1523
267
00:10:52
23.10.2019

#kukuwengi #ufugaji #kienyeji

Njia Rahisi ya Kupata Vifaranga 200 Wa Kienyeji Kwa Muda Mfupi

16565
156
24
00:09:39
08.05.2021

Ufugaji wa kuku wa kienye ni safari ndefu inayohitaji utaalam, umakini, ubunifu na uvumilivu ili uweze kufuga kisasa na kuongeza tija kwenye ufugaji wako. Watu wengi ambao huanza ufugaji wa kuku wa kienyeji huanza na kuku wachache, wakitegemea kupata vifaranga wengi wa kienyeji ili kukuza miradi yao. Sasa kwenye Makala ya leo tutajifunza Njia rahisi ya kupata vifaranga wengi wa kienyeji kwa muda mfupi. Nimekusanya vifaranga 200 wa kienyeji ndani ya miezi miwili na lengo nifikishe vifaranga 300 ndani ya miezi 3 nikiwa na matetea 38. #vifarangawakienyeji #kukuwakienyeji #ufugajiwakukuwakienyeji

NJIA YA KUPATA KUKU WENGI WA KIENYEJI KWA MUDA MFUPI 2020

56619
413
43
00:13:54
27.05.2019

Njia ya kupata kuku wengi wa kienyeji kwa muda mfupi, nimaelezo ya kina yanayokupa mwanga wewe kama mfugaji wa kuku wa kienyeji njia rahisi ya kupata vifaranga wengi kwa muda mfupi. mbinu hii ya asili inaufanisi wa zaidi ya 95% katika kuleta matokeo chanya kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. kama changamkia fursa Tv tunashauri Wafugaji watumie mbinu hizi ili wakue kiuchumi na kuongeza kipato Chao. Tags: njiaa ya kupata kuku wengi kwa muda mfupi, kutotolesha mayai kwa njia ya asili, kuku wa kienyeji, ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbinu bora ya ufugaji wa kuku, kutotolesha mayai ya kuku kwa kutumia pumba, mbinu bora za ufugaji wa kuku, vifaranga vya kuku wa kienyeji, chanjo ya vifaranga wa kienyeji, ufugaji wa kuku, changamkia fursa Tv, kupata kuku wengi wa kienyeji

Jinsi ya Kutunza Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji

195193
980
138
00:08:19
18.07.2021

jinsi ya kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji Ufagaji wa vifaranga vya kuku wa kienyeji una changomoto nyingi, wafugaji wengi wamekuwa hawajui mbinu ambazo zitawasadia kuweza kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji katika mbinu ambazo zitawafanya vifaranga wasife. kama nawe ni miongoni mwa wafugaji hoa, siku ya leo nitakupa mbinu bora za kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji.

Nilianza na Kuku 8 wa Kienyeji, Lakini Nimezalisha Kuku wa Kienyeji 300

234114
1077
165
00:10:37
07.07.2021

Nilianza na Kuku 8 wa Kienyeji, Lakini Nimezalisha Kuku wa Kienyeji 300 🤍fursatv Katika mfululizo wa vipindi vyetu vya ufugaji wa kuku hapa changamkiafursa, tunahitaji kumuinua mfugaji wa kuku wa kienyeji aache kufuga kuku kwa mazoea na aanze kufuga kuku wa kienyeji kibiashara. Ili ufuge kuku wa kienyeji kibiashara unatakiwa kuwa na makoo yasiyopungua 250 na sio rahisi kwa Wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho. Sehemu 1: 🤍 Sasa ili kulikamilisha hilo mfugaji anapaswa kuwa na uwezo wa kuzalisha vifaranga wengi wa kienyeji kwa pamoja, ambavyo vitampa mfugaji hamasa ya kuweka nguvu kubwa kwenye uleaji vifaranga kitu ambacho kitachangia ongezeko kubwa la idadi ya kuku wa kienyeji na kuleta tija kibiashara. Kufanikisha zoezi hili mfugaji anapaswa kuandaa vitu vifuatavyo:- 1. Banda bora na litakalo endana na idadi ya kuku anaohitaji kufuga. 2. Makoo na jogoo (Makoo ni kuku ambao wametaga angalau mara moja). Makoo watasaidia kupunguza muda wa kusubiri ili kuliona yai la kwanza. 3. Vifaa vya maji, chakula na Chumba maalumu cha kulelea vifaranga 4. Makasha au box la kutunzia mayai 5. Elimu ya ufugaji bora wa kuku, itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za mradi wako Baada ya kukamilisha maandalizi hayo, sasa twende tukaanze kuzihesabu hatua za awali za kufata ili kukusanya vifaranga wengi kwa pamoja na baadae uleaji wa hao vifaranga watakaokuwa kuku wa baadae.

SHAMBANI: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

164998
887
62
00:24:48
17.11.2020

SHAMBANI: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

NJIA RAHISI YA KUPATA VIFARANGA WENGI WA KUKU WA KIENYEJI 2021

267866
2896
174
00:10:15
04.03.2020

Njia rahisi ya kupata vifaranga wengi wa kienyeji kwa muda mfupi. Katika mfululizo wa vipindi vyetu vya ufugaji wa kuku, tunahitaji kumuinua mfugaji wa kuku wa kienyeji aache kuishi na kuku na aanze kufuga kuku wa kienyeji kibiashara. Ili ufuge kuku wa kienyeji kibiashara unatakiwa kuwa na makoo yasiyopungua 250. Sio rahisi kwa Wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na mtaji mkubwa kiasi hicho. Ili Kujifunza zaidi tafadhali tazama video hii 🤍 Kufanikisha zoezi hili mfugaji anapaswa kuandaa vitu vifuatavyo:- 1. Banda bora na litakalo endana na idadi ya kuku anaohitaji kufuga. 2. Makoo 20 na jogoo 3 - 4 (Makoo ni kuku ambao wametaga angalau mara moja). Makoo watasaidia kupunguza muda wa kusubiri ili kuliona yai la kwanza. 3. Vifaa vya maji, chakula, joto na bruda 4. Chumba maalumu cha kulelea vifaranga 5. Makasha ya kutunzia mayai 6. Elimu ya ufugaji bora wa kuku, itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za mradi wako Hatua 1; Nunua koo 20 na jogoo 3 - 4 kutoka kwa Wafugaji unao wafahamu. Jitahidi kununua hao kuku kutoka sehemu tofautitofauti ili kuepuka magonjwa ya kurithi kizazi hadi kizazi. Chagua koo na jogoo wenye maumbo makubwa na wenye afya ili kupata mbegu bora na inayokuwa haraka. Ukiwafikisha bandani, wape antibiotics kwa siku 5 kwaajili ya tahadhari ya magonjwa ya bakteria. Wasipo onyesha ugonjwa wowote, wape chanjo ya kideri/Mdondo (Newcastle disease Vaccine) na utunze kumbukumbu kwaajili ya kurudia chanjo hiyo kila baada ya miezi 3. Hatua 2; Watenge hao kuku katika ratio ya 1:6 au 1:7, yani jogoo 1 na majike 6 au 7 ili kuwa na urutubishaji mzuri wa mayai yatakayokupa vifaranga wengi na wenye ubora. Pia kuwatenga kila jogoo na Koo wake katasaidia kupunguza majogoo kupigana na kuwafanya warutubishe mayai vizuri. Hatua3; Baada ya wiki 2 - 3 kuku wataanza kutaga. Nunua mayai ya kisasa na uyawekee alama kisha uyaweke kwenye viota na kila siku kuku anapotaga yai, lichukue kisha liandike tarehe ya kutagwa na ulihifadhi kwenye makasha uliyoyaandaa. Zingatia kuweka mayai 2 ya kisasa kwenye kila kiota cha kuku anaetaga. Fanya hivyo kwa kila kuku atakae taga. Uhifadhi wa Mayai I. Mayai yahifadhi kwenye makasha ya boksi (trays) huku sehemu ya yai iliyochongoka ikiwa Chini na sehemu ya duara ilkiwa juu. II. Mayai yahifadhiwa kwa mstari kufatisha siku ambayo yai lilitagwa. III. Yahifadhi sehemu yenye mwanga hafifu, Joto la kawaida la chumba (Room temperature 25°C) na hewa ya kutosha ili yasiharibike. Maranyingi tunahifadhi chini ya uvungu wa kitanda (Zingatia usafi wa chumba) IV. Mayai kwaajili ya kuatamiza hayatakiwi kuzidisha Siku 14 kabla ya kuatamiwa. Mfano kuku akitaga mayai 16, mtolee mayai mawili ya kwanza kutagwa kwa sababu yatakuwa yamezidisha siku 14. Hatua 4; Baada ya muda wa siku kadhaa kuku wataanza kuatamia, waachie yale mayai ya kisasa tuliyoyaweka mwanzo wa yaatamie tukisubiri idadi ya kuku wanaotaka kuatamia ifike 14 -15. Wakifika kuku 14 - 15 wanaotaka kuatamia, muda wa usiku kama saa 1 au saa 2 hivi, ingia bandani na mayai tuliyoyatunza awali. Ondoa mayai yote ya kisasa na umuwekee kila kuku mayai 14 - 15 ambayo hayajazidisha siku 14 tangu yatagwe. Siku hii tutaihesabu kama ni siku ya kwanza ya mayai yetu kuatamiwa. Kwa maana hiyo tutakuwa tumeatamiza mayai 196 - 225, ambayo yakitotoka kwa 90% tunatarajia vifaranga 176 - 200 baada ya siku 21. Uchaguzi wa Mayai Bora ya Kuatamisha I. Mayai yawe yamerutubishwa na jogoo (zingatia uwiano 1:6 au 1:7) II. Chagua Mayai yenye ukubwa wa wastani, mayai makubwa au madogo kuliko wastani hayatoi kifaranga III. Chagua mayai masafi, yasiyokuwa na kinyesi au damu na yasiwe na nyufa IV. Chagua mayai yenye umbo la kawaida ( Oval shape), mayai ya duara au yaliyochongoka kuliko kawaida hayatoi kifaranga. Hatua 5; Wiki moja kabla ya kupokea vifaranga, andaa chumba cha kulelea vifaranga. Kisafishe vizuri na kisha pulizia dawa ya kuua vimelea vya magonjwa kwa kutumia disfectant ( V-rid au D4) ili kuzuia magonjwa nyemelezi kwa vifaranga wako. Andaa bruda na vifaa vingine vya kulelea vifaranga kama jiko au chungu cha joto, mkaa, magazeti na matandiko (maranda au pumba ngumu ya mpunga) Andaa chakula, antibiotics na vitamin za kuwaanzishia vifaranga Hatua 6; Baada ya siku 21, kuku wote walioatamia watatotoa vifaranga na kama urutubishaji wa mayai ulikuwa mzuri utapata vifaranga 170 - 200. Baada ya kusikia sauti za vifaranga, pasha joto chumba ulichoandaa hatua ya 5 masaa 4-6 kabla ya kuingiza vifaranga. Hii itawafanya vifaranga wahisi joto kama wako na mama yao (zingatia joto kama tulivyoeleza kwenye kitabu hiki). Ingiza vifaranga kwenye bruda baada kupata joto na taratibu zingine za uleaji wa vifaranga ziendelee kama kitabu hiki kinavyoeleza. Usisubiri kuku atoe vifaranga mwenyewe ndio umnyang'anye, atasumbua kutafuta vifaranga vyake. Pia unaweza kumpatia mayai mengine aatamie ili upate vifaranga wengine baada ya siku 21. Ukifanya hivyo wape chakula cha kutosha na maji safi na salama. #ufugajiwakukuwakienyeji

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI BIASHARA | Biashara ya Kuku wa Kienyeji

33117
322
25
00:10:05
01.05.2020

Katika ukuaji wa biashara ya kuku, kuku wa kienyeji bado soko lake liko juu na kwa kulitambua hilo, changamkia fursa inakuletea video ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara, itakayokuwezesha kufuga kuku wa kienyeji kwa faida kubwa na ya uhakika. Binafsi ni mfugaji pia wa kuku wa kienyeji na chotara na mbinu hizi hunisaidia kuingiza kipato cha Milioni 3 kwa mwaka kupitia kuku wa kienyeji. Mbinu hizo ni kama zifatazo: 1. Kuzalisha vifaranga bora 2. Jinsi ya kuwalisha Wiki 1-2 broiler stater Wiki 3-8 chick start Wiki 9 - 18 Grower Wiki 19-20 layers 3. Umri wa kuwatoa bandani PLAYLIST Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji 🤍 Ufugaji wa Kuku Chotara 🤍 Magonjwa Tishio ya Kuku 🤍 Ujenzi wa Banda Bora 🤍 Uleaji Bora wa Vifaranga 🤍 SOCIAL MEDIA YouTube; 🤍 Facebook; 🤍 Instagram; 🤍 Twitter; 🤍 What's app; 255 (0)752209073 For Business Purposes Email; changamkiafursa🤍gmail.com

Ujenzi wa Banda la Vifaranga wa Kuku wa Kienyeji

96971
541
73
00:09:52
07.09.2021

Ujenzi wa banda la kutunzia Vifaranga wa Kuku wa kienyeji. Ili vifaranga wa kienyeji wakue bila changamoto za vifo kama mfugaji wa kuku haupaswi kusahau ujenzi wa banda la kulelea vifaranga. Banda la vifaranga ni sehemu muhimu sana katika ufugaji wa kuku wa kienyeji. Vifo vingi vinavyotokea kwenye kuku wa kienyeji ni kwa sababu ya wafugaji hawaandai banda la kulelea vifaranga hivyo wanawaacha kuku wazunguke na vifaranga wao mchana kutwa bila kufikiria hatari ya wanyama na ndege wa porini waonaowahitaji hao vifaranga kama kitoweo. Sasa kwenye makala ya leo tutajifunza Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda la kulelea vifaranga wa kienyeji. #jinsiyakutengenezabandalavifarangawakienyeji

Jinsi ya Kuanza Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Ep2

75328
380
36
00:07:36
08.09.2019

ufugaji wa kuku wa kienyeji na jinsi ya kulea vifaranga vya kuku

Ufugaji wa kuku wa mayai layers;Mambo saba muhimu ya kuzingatia ili ufuge kuku wa mayai kwa faida.

33077
198
42
00:06:19
28.07.2021

Jifunze mambo muhimu ya kuzingatie ili ufuge kuku wa mayai kwa tija. #mkulimasmart #shambadarasa UFUGAJI WA KUKU:Je mfugaji mdogo ufuge kuku wa nyama ... Ufugaji wa Kuku wa Mayai | Sababu 6 Zinazosababisha ... Mchanganuo wa Ufugaji wa Kuku wa Mayai *MWONGOZO WA KUKU WA MAYAI NAMNA BORA YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI UFUGAJI WA KUKU WA KISASA WA MAYAI BRAND POULTRY FEED: DARASA LA UFUGAJI Ufugaji wa Kuku wa Mayai - Sehemu ya Tano (Layer Poultry ... UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI HATUA KWA HATUA | ufugaji wa kuku wa mayai wa kienyeji mtaji wa kuku wa mayai biashara ya kuku wa mayai mchanganuo wa ufugaji wa kuku wa mayai gharama za ufugaji wa kuku wa mayai chakula cha kuku wa mayai bei ya kuku wa mayai ufugaji wa kuku wa mayai pdf

Sasa Nafuga Kuku Chotara Kibiashara, Zaidi ya Kuku 700 wa Rika Tofauti

82654
500
46
00:07:02
23.01.2021

Ufugaji wa Kuku Chotara Kibiashara ni safari ya inayohitaji uvumilivu, Ufugaji wa kuku sio upatu, wala sio safari ya kulala masikini na kuamka tajiri. Kufanikiwa kwenye ufugaji wa kuku chotara ya kupasa uwetayari kuwekeza muda na pesa zako kwa muda wa miezi 6 au zaidi kabla ya kuyaona mafanikio. USIBONYEZE: 🤍

UJENZI WA BANDA BORA LA KUKU KIENYEJI | CHOTARA | MAYAI | NYAMA / BROILER

256473
1776
200
00:13:00
16.11.2019

Ujenzi wa Banda Bora la Kuku | Kuku chotara | Kuku wa Kienyeji | Kuku wa Mayai | Kuku wa Nyama. Ni video inayofundisha namna ya ujenzi bora wa kuku aina zote. Kwenye video hii utajifunza 1. jinsi ya kupata ukubwa wa banda kwa aina zote za kuku 2. Malighafi za kutumia 3. Vipimo vya urefu na upana

KUKU WA KIENYEJI Ili WAKULIPE ZAIDI Fanya Yafuatayo

70861
1003
55
00:10:05
15.04.2020

#kukuvillage #kienyeji #chickenkeeping

Jinsi ya kupata kuku wengi wa kienyeji

225800
1776
473
00:10:46
12.04.2021

✍️Mbinu hizi mbili zitakusaidia kupata kuku wengi wa kienyeji (a)Kumwekea mayai mengine kuku aliyetoka kutotoa na kuvilea vifaranga (b)Kumfungia kuku aliyetotoa na kuvilea vifaranga

NILIANZA NA KUKU 2 TU WA KIENYEJI - SASA HIVI NINA KUKU CHOTARA 500

202783
1191
164
00:10:13
25.01.2020

NILIANZA NA KUKU 2 TU WA KIENYEJI - SASA HIVI NINAFUGA KUKU CHOTARA 500 Hakuna wa kumlaumu unaposhindwa kufikia malengo yako kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji Bi: Anthonia Lymo alianza ufugaji wa kuku mwaka 2015 akiwa na kuku wa Wili tu wa kienyeji, lakini sasa anafuga kuku chotara zaidi ya 500. Anatengeneza laki 7 kila wiki kwa biashara ya uuzaji wa vifaranga bora vya kuroiler. Endelea kufatilia changamkia fursa, tutakuhamasisha na kuku fundisha mbinu bora za ufugaji wa kuku.

Njia Rahisi ya Kutengeneza FUNZA wa kuwalisha Kuku wa Kienyeji Kwa Kutumia Pumba za Mahindi.

103046
621
86
00:13:05
24.05.2020

kukuvillage #kienyeji #chickenkeeping

Utunzaji wa Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji BILA VIFO

31132
210
14
00:08:05
11.02.2022

Muongozo wa Uleaji wa Vifaranga wa Kienyeji Mfugaji ni vizuri ujiandae kupokea vifaranga kama ambavyo hua unajiandaa kupokea mtoto kabla ya kujifungua. Maandalizi hayo ni kama yafuatayo:- 1. Baada ya ujenzi wa banda kukamilika, banda lifanyiwe usafi wiki mbili kabla ya kuingiza vifaranga. 2. Wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga, matandiko yaliyosafishwa kuondoa vumbi yawekwe bandani, na banda zima lipuliziwe dawa (disfectant). Hakikisha kimo cha matandiko ni angalau inch 3 3. Tengeneza bruda kwaajili ya kuzuia joto lisipotee na andaa vifaa vya maji, chakula na magazeti yatakayo tandikwa juu ya Matandazo ndani ya bruda kuwasaidia vifaranga kutofautisha chakula na matandazo. N.B: Badilisha magazeti hayo kila unapoona yamechafuka ndani ya siku 3-4 za mwanzo ambao atakua mwisho wa matumizi. 4. Kabla vifaranga kuingi bandani, bruda lipashwe joto kwa masaa sita huku vifaa vya maji yenye glucose na vitamin vikiwa ndani ya bruda. Baada ya masaa hayo vifaranga waingizwe bandani na kuruhusiwa kunywa maji yenye glucose kwa masaa 2 mfululizo. 5. Hakikisha Kuna joto la kutosha muda wote ndani ya bruda ili kuzuia ugonjwa wa vichomi (Pneumonia). Unaweza kutumia vyungu, bulb ya 100w, chemli au vifaa vingine vya umeme au gesi.

JINSI YA KUWALISHA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI WAKUWE HARAKA

48681
614
85
00:07:36
01.08.2020

Jinsi ya kuwalisha vifaranga wa Kuku wa kienyeji Wakuwe Haraka Kuna baadhi ya Watu hawapendi kufuga kuku wa kienyeji kwa kusingizia kuwa wanachelewa kukuwa na vifaranga wa kienyeji wanashambuliwa sana na magonjwa, sasa kwenye kipindi cha leo nitakuelekeza jinsi kuwalisha vifaranga wa kuku wa kienyeji ili waepukane na magonjwa na wakue haraka uwahi kuwauza na upate faida. Stay tuned Tatizo kubwa la vifaranga vya kuku wa kienyeji kushambuliwa na magonjwa, kudumaa na kuchelewa Kukuwa ni chakula. Wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji huwapa kuku chakula ambacho sio mlo kamili (Balance Diet) Mlo kamili (Balance Diet) ni chakula ambacho kinavirutubisho vyote muhimu kwaajili ya Kulinda mwili dhidi ya magonjwa, Kuupa mwili nguvu, kujenga mwili, kuupa mwili joto, kuimarisha mifupa na kusafisha na kurahisisha mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri Unaweza ukajiuliza ni vyakula gani hivyo ambavyo vinafanya kazi zote hizo mwilini? Usipate shida, nitakufundisha kila kitu kwenye video hii. Chakufanya kama ndio mara ya kwanza kutazama video za channel hii basi Subscribe na kisha bonyeza alama ya kipengele itakayojitokeza, pia usisahau ku-Like na share ili Tuwafikie Wafugaji wengi. Vilevile unaweza kuuliza chochote kwenye comment na sisi tutakujibu. Vyakula hivyo ambavyo huchanganywa na kukupa mlo kamili wa kuku wa kienyeji ni kama vifatavyo Vyakula vya Kulinda mwili dhidi ya magonjwa ni Vitamin ambayo hutokana na Mimea kama Azolla, hydroponics, mchicha, Lucina na mimea yote ya kijani au unaweza kuchanganya ambayo imeandalia maalumu (premix) Vyakula vya Kuupa mwili nguvu ni Carbohydrates/Wanga ambayo hutokana na nafaka kama mahindi, mtama, ngano, na pumba zote za nafaka Vyakula vya kujenga mwili ni Protein ambayo hutokana na mashudu ya alizeti, karanga na pamba, Soya, Dagaa (Fishmeal) na damu ya wanyama iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya chakula cha kuku Vyakula vya kuupa mwili joto ni Fats/ Mafuta vyakula Vyenye mafuta kama Alize, karanga, pamba, nazi na mashudu ya vyote nilivyotaja Vyakula vya Kuimarisha mifupa ni Madini mbalimbali ambayo hutokana na Unga wa mifupa ya wanyama na samaki na Chokaa kama Calcium, Iron, Phosphorus, Zinc n.k Na Maji safi na salama, ambayo Husafisha na kurahisisha mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri Vyakula vyote nilivyo taja vikichanganywa kwa utaratibu maalumu na kutengeneza Digestible Crude Protein (DCP) ya 18% - 20% chakula hicho kinaitwa stater/Chick Mash ambacho wanapewa vifaranga walio na umri wa siku 1 mpaka wiki 8 na wanatakiwa kulishwa kwa utaratibu maalumu . Utaratibu wa kuwalisha vifaranga wa kienyeji ni kama ufatao. Wiki ya 1 na 2 walishe chick stater bila kuwapimia, wape wale tuu kadri watakavyo chakula kikiisha kwenye feeder waongezee. Kufanya hivyo kutawasaidia kuimarisha kinga ya mwili ili kuwaepusha na magonjwa nyemelezi, kujenga mwili na vifaranga watakuwa kwa haraka. Ukiweza kumudu gharama kwa kipindi hiki cha siku 14, walishe stater ya pillet vifaranga watakula chakula chote bila kubakisha na wataimarika kwa haraka sana. Wiki ya 3 mpaka wiki ya 7, endelea kuwalisha Vifaranga stater lakini ukiwa unapima kiasi cha kuwapa kwa siku husika. Wiki ya 3 wape gramu 25 Wiki ya 4 wape gramu 31 Wiki ya 5 wape gramu 36 Wiki ya 6 wape gramu 41 Wiki ya 7 wape gramu 45 Wiki ya 8 wape gramu 49 Wiki hii ya 8 ni wiki ambayo unatakiwa kuanza kuwazowesha chakula cha grower mash kwa kuchanganya kiasi kidogo kidogo kwenye stater ya siku husika. Mfano kama vifaranga wanakula kilo 5 kwa siku, changanya stater kg 4 na grower kg1. Endelea kuongeza grower na punguza stater mpaka itakapokuwa imeanza wiki ya 9, chakula chako kiwe ni grower mash pekee. Ukiwalisha Vifaranga wako kwa utaratibu huu utaona matokeo ya ukuaji wao na jinsi ambavyo hawatakuwa wakishambuliwa na magonjwa. Nikualike kwenye darasa la ufugaji wa kuku aina zote litakalo anza tarehe 10 mwezi wa 8, darasa linafanyika Mtandaoni kupitia group la what's app. Kujiunga na darasa hilo tuma 5,000 kwenye namba unayoiona kwenye screen 0656528455, kisha tuma meseji ya jina na namba yako ya what's app.

Nimeweza Kufuga Kuku wa Kienyeji Kibiashara, Usiache Kujaribu Hawa Kuku ni Biashara

28308
218
37
00:09:15
30.11.2021

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara, umegubikwa na maneno mengi sana ya kukatisha tamaa. Maneno kama kuku wa kienyeji wanakua taratibu sana, hawana uzito mkubwa, wanataga mayai machache, gharama za chakula zinaenda juu zaidi. Wapo waliokata tamaa kwa kusikiliza maneno hayo, lakini tupo tulioamua kuziba masikio na kukomaa kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na inatulipa. Niliamua kufanya utafiti kupitia maneno yanayo sambaa kuhusu ufugaji kuku wa kienyeji na kile nilichokipa nimekielezea kwenye video hii. Tazama mpaka mwisho ujifunze mengi kutoka changamkia fursa. #kukuwakienyejiwanalipa #ufugajiwakukuwakienyejikibiashara #kukuwakienyejinibiashara

JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU BILA KUPATA V I F O

104560
864
96
00:10:35
04.11.2020

Jinsi ya kulea vifaranga vya kuku bila kupata vifo USIBONYEZE: 🤍

UFUGAJI KUKU UNAOWASHANGAZA WENGI, NI MRAHISI NA UNALIPA MARA DUFU KWA MFUGAJI.

38769
176
17
00:16:07
17.02.2021

Karibu utazame chaneli yako pendwa ya Star TV Africa. Jiunge nasi kupata habari za kitaifa na kimataifa, makala, burudani na habari za michezo katika nyanja zote! Kutoka Ilemela - Mwanza, Tanzania mpaka ulipo, TUNAKUFIKIA! Star TV Brightens Your Day !

Назад
Что ищут прямо сейчас на
ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa Genshin Card Game ТРЕНДЫ ТИКТОК Borja Mayoral zabbix snmp linux ВСЕ МАЙНКРАФТ ПЕСНИ ФИКСАЯ И ФИКСПЛЭЯ ROSALÍA NEW VIDEO raspberry pi 4 Viking Grace khabane lame osu!mania осу! cschdfcbankloan BMC Official Video Как продавать на Wildberries moza �������������� IRP using davinci resolve visualizer